Manchester United yapigwa na West Ham United, Yafungashwa Virago



KLABU ya Manchester United inayonolewa na Kocha Mkuu, Ole Gunnar Solskjaer imefungashiwa virago katika Kombe la Carabao katika raundi ya tatu baada ya kukubali kupoteza mbele ya West Ham United.
Ikiwa Uwanja wa Old Trafford mbele ya mashabiki 72,568 ilinyooshwa mapema dakika ya 7 na mtupiaji alikuwa ni Manuel Lanzini bao lake lilitosha kuipa ushindi timu yake ya West Ham United.

Solskjaer alitoka kumnyoosha West Ham United mabao 2-1 katika mchezo wa Ligi Kuu England akiwa ugenini katika Uwanja wa London naye amepoteza mbele ya Kocha Mkuu David Moyes ambaye anashinda kwa mara ya kwanza mbele ya United Uwanja wa Old Trafford kwa kuwa mara ya mwisho kwa timu hiyo kupata ushindi mbele ya United ilikuwa ni 2007 na mtupiaji alikuwa ni Carlos Tevez.

Solskjaer ameweka wazi kuwa walianza vibaya na walishindwa kutengeneza nafasi kubwa zaidi ya kutoa presha kwa kuwa walipiga mashuti 27 huku wapinzani wao wakipiga mashuti 9. West Ham United inakwenda kukutana na Klabu ya Manchester City katika hatua ya 16 bora.

Rekodi zinaonyesha kuwa Manchester United walipiga jumla ya mashuti 27 na ni 6 yalilenga lango huku West Ham United wakipiga mashuti 9 na matatu yalilenga lango.


Post a Comment

0 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.

Top Post Ad

Below Post Ad