Marekani imetangaza kuondosha marufuku ya kusafiri iliyowekwa kwa ajili ya kukabiliana na janga la Covid-19 kwa abiria wote waliokamilisha chanjo, kufanya vipimo na kufahamika mwenendo wao.
Vizuzuzi hivyo vikali kuwahi kushuhudiwa vilikuwa vimewazuia ndugu, jamaa, marafiki na wafanyabiashara dunani kote na kutenganishwa kwa miezi mingi katika kipindi hiki ambacho janga hilo likiendelea.
Mratibu anayehusika na masuala ya virusi vya corona wa Rais Joe Biden, Jeffrey Zients, amewaambia waandishi wa habari hatua hiyo itaanza kutekelezwa Novemba.
Lakini hatua kadhaa zitaendelea kubaki, kwa lengo la kudhibiti kuenea kwa virusi ambavyo vimewauwa Wamarekani zaidi ya 675,000 na wimbi lake liliibuka tena mapema mwaka huu baada ya wengi kudhani limekwisha.