Masau Bwire Aajiriwa Hapa





SHIRIKISHO la Mpira wa Miguu kwa Walemavu (TAFF) limemteua Masau Bwire kuwa Mkuu wa Idara ya Habari na Mawasiliano na balozi wa shirikisho hilo.

Uteuzi wa Masau ambaye anashika nafasi kama hiyo kwenye klabu ya Ruvu Shooting umekuja kama sehemu ya kuongeza hamasa kwa wadau kuelekea kwenye mashindano ya Africa CANAF yatakayofanyika hapa nchini mwaka huu.

Rais wa TAFF Peter Sarungi alisema: “Tulimuomba Masau kuwa balozi wetu kwa sababu ni mtu mwenye ushawishi na kwa bahati tulivyompa ombi letu hili hakukataa na akakubali kuungana na sisi.”

Naye Masau aliliambia Championi Jumatano kuwa: “Watu watashangaa kwa nini nimekubali kazi hii, kwa sababu silipwi hata punje ya hela. Kubwa ni uzalendo na upendo wangu kwa michezo hususan kwa watu wenye ulemavu.”

Naye Katibu Mkuu wa TAFF, Mosses Mabula alitumia nafasi hiyo kueleza kuwa Tanzania itakuwa mwenyeji wa mashindano ya Afcon yatakayoanza kufanyika Novemba 25 hadi Desemba 5 na nchi 15 zimekubali kushiriki.

“Mashindano yatafanyika kwa siku 10 pekee na viwanja viwili kwa maana ya Uwanja wa Uhuru na Mkapa ndivyo vitatumika. Nchi kama Misri, Angola, Liberia, Rwanda na zingine tukiwemo sisi Tanzania tutashiriki.”

Post a Comment

0 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.

Top Post Ad

Below Post Ad