Mashahidi 20 Kesi ya Sabaya





KUTOKA ARUSHA: Aliyekuwa Mkuu wa Wilaya ya Hai, Lengai Ole Sabaya na watuhumiwa wenzake sita wanaoshtakiwa katika kesi ya uhujumu uchumi wameanza kusomewa maelezo ya awali huku upande wa Jamhuri ukitarajia kuleta mashahidi 20 na vielelezo 16 vya mashtaka hayo.

Sabaya na wenzake wanashtakiwa kwa shtaka la uhujumu Uchumi lenye makosa mbalimbali ikiwemo kuongoza genge la uhalifu na utakatishaji wa fedha.

Akiwasomea maelezo hayo ya awali jana Alhamisi, Septemba 16, 2021, Wakili wa Serikali mbele ya Hakimu Mkazi, Dkt Patricia Kisinda amesema Sabaya akiwa na wenzake sita walielekea kwenye gereji ya Mroso iliyopo Kwa Mworombo, Arusha na kumtuhumu mfanyabiashara Francis Mroso kuingiza bidhaa kutoka Nairobi, Zanzibar na Dubai bila kulipa kodi.

Wakili Mkuu wa Serikali, Tumaini Kweka amesema wanatarajia kuwa na mashahidi 20 pamoja na vielelezo 16 kwenye kesi hiyo ambapo Hakimu ameiahirisha kesi hiyo hadi September 23 na 24, 2021.

Post a Comment

0 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.

Top Post Ad

Below Post Ad