BAADA ya kikosi cha Yanga kupoteza katika mchezo wa awali wa Ligi ya Mabingwa Afrika dhidi ya Rivers United, uongozi wa timu hiyo umeweka wazi kuwa bado una nafasi ya kupata matokeo katika mchezo wa marudio.
Katika mchezo uliochezwa jana Septemba 12, baada ya dakika 90, ubao wa Uwanja wa Mkapa ulisoma Yanga 0-1 Yanga jambo lililowapa maumivu mashabiki pamoja na Watanzania kiujumla.
Bao pekee la ushindi lilipachikwa na Moses kwa kichwa akiwa ndani ya 18 baada ya kipa namba moja wa Yanga, Diarra Djigui kutoka kidogo katika eneo lake.
Haji Manara, Ofisa Habari wa Yanga ameweka wazi kuwa kuna dakika 90 za kupambana.
"Tunazo dakika rising nyingine za kupambania timu yetu, chini yanjua hili hakuna kisichowezekana. Tupeane pole kwa matokeo lakini tusikate tamaa,"
Katika mchezo wa jana rekodi zinaonyesha kuwa Yanga ilipiga jumla ya kona 7 huku Rivers United wakipiga kona moja na Yanga ilipiga jumla ya mashuti 13 na ni moja lililenga lango huku Rivers United ikipiga mashuti 11 na ni mawili yalilenga lango.