Naibu wa Rias nchini Kenya William Ruto amemjibu waziri wa msuala ya ndani nchini Kenya Fred Matiangi kufuatia matamshi ya kamati moja ya bunge siku ya jumatano.
Kulingana na taarifa ilitolewa na msemaji wake David Mugonyi, na kunukuliwa na gazeti la The People Daily nchini Kenya, naibu huyo amemkosoa waziri Matiangi kwa kutoa matamshi yasio na msingi.
Kulingana na naibu huyo lengo la Matiangi katika kikao hicho cha kamati ya bunge lilikuwa kundhalilisha na kumkejeli yeye na afisi yake.
‘’Kulingana na matamshi yaliotolewa na waziri Matiangi hakuna Ushahidi kwamba anataka kuelewa katiba ama hata wasiwasi uliopo kuhusu usalama wa naibu wa rais’’, alisema Mugonyi.
‘’Bwana Matiangi ametumia vibaya rasilimali ya umma na uwezo wa ofisi yake kwa maslahi ya kisiasa ili kumdhalilisha na kuikejeli ofisi ya William Ruto kwa propaganda za kisiasa’’, aliongezea.
‘’Kulingana na naibu William Ruto , waziri huyo wa masuala ya ndani amejaribu kuonesha kwamba ofisi ya naibu huyo haihitaji huduma kutoka kwa ofisi yake’’.
Kulingana na Gazeti la The People,amemshtumu Matiangi na kusema hatua yake inahatarisha usalama wa maisha ya naibu wa rais William Ruto.
‘’Kwa kumtaja naibu wa rais na usalama unaopatiwa mali yake, waziri Matiangi aliibagua ofisi ya naibu huyo na hivyo basi kuhatarisha Maisha yake’’ , aliongezea Mugonyi.