Mchungaji Cyril Utomi kutoka Nigeria ameyachoma mawigi na vipodozi vya muumini wa kike kwa madai asingeweza kukutana na Yesu akiwa na nywele na vitu vingine vya bandia ikiwa ni pamoja na viatu virefu.
Picha ya Mchungaji Cyril Utomi
Utomi alichoma vitu hivyo katika mkutano wa mahubiri ulioandaliwa na Holiness Revival Movement Worldwide mwishoni mwa mwezi Agosti na baada ya tukio hilo aliamua ku-post picha zinazoonesha vitu hivyo vikiteketea kwa moto katika mtandao wa facebook