Meli ya kubeba ndege ya Queen Elizabeth yatia nanga Japan



 
Meli ya kubeba ndege ya Queen Elizabeth yatia nanga Japan
Meli ya kubeba ndege Uingereza ya Queen Elizabeth ilitia nanga huko Japan kwa mara ya kwanza.

Kikosi cha maamlum na meli ya kubeba ndege ambayo ilisafiri kutoka Uingereza mnamo Mei, ilifika Yokosuka, kituo cha baharini cha Marekani kilichoko kusini mwa mji mkuu wa Tokyo.

Kamanda wa Kikosi maalum Steve Moorhouse alielezea ziara hiyo katika ujumbe wake kwenye Twitter kuwa kama kujitolea kwa Uingereza "kuimarisha uhusiano wa kidiplomasia, uchumi na usalama katika Indo-Pacific" na "kuchukua uhusiano uliopo kwa kiwango kipya" na Japan.

"Uwepo wa meli hizo ni mfano wa uungwaji mkono wa Uingereza kwa uhuru na usalama wa njia muhimu za kibiashara katika eneo hilo na mfumo wa kimataifa ambao utafaidisha nchi zote," Moorhouse alisema.


 
Kikosi maalum kitaondoka Japan Septemba 9.

Ripoti ya shirika la utangazaji la umma NHK ilisema kwamba ziara hiyo "itaimarisha uhusiano wa kijeshi wa nchi husika na Japan, ambayo Uingereza inaona kama mshirika wake wa karibu zaidi wa usalama huko Asia."

Inajulikana kuwa meli ya Queen Elizabeth, ambayo ilianza kuhudumu rasmi mnamo 2017 na kutambulika kama mbebaji mkubwa zaidi wa ndege huko Uingereza, ina uwezo wa kupakia ndege 40.

Tags

Post a Comment

0 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.

Top Post Ad

Below Post Ad