Nafahamu fika bila shaka mawasilaiano ya simu yamekusaidia mambo mbalimbali.
Pamoja na kukusaidia mambo hayo mbalimbali swali langu kwako je umfahamu mgudunzi wa simu?
Kama jibu ni hapana, basi fahamu ya kwamba bwana Alexender Graham Bell huyu ndiye mgunduzi wa simu ya kwanza kabisa.
Alexender Graham Bell yeye alizaliwa mnamo mwaka 1847 katika mji wa Edinburgh nchini Uskoti na baadae alihamia nchi za kanada.
Baba yake na mgunduzi huyu wa simu alikuwa ni mwalimu wa wanafunzi wenye ulemevu wa kusikia yaani viziwi baadae elexender naye ajilijikuta anakuwa na mgunduzi na mvumbuzi wa vitu mbalimali.
Wakati mkewe ndiye aliye mvutia na kumshawishi Alexander Graham Bell aweze kuzama ndani zaidi kiuchunguzi kwa kufanya uchunguzi katika matamshi na usikilizaji baadae alikwenda zaidi kuchunguza ni jinsi gani vifaa vya kusikilizia sauti hufanya kazi hapo ndipo alipo weza kuibuka na simu yakwanza yenye kufanya kazi.
Alizawadiwa tuzo iliyo fahamika kama first U.S patent mnamo mwaka 1876, pia ukimbuke mwaka huu ndio alifanikiwa zoezi la kugundua simu yake ya kwanza, pamoja na hayo alikataa kutumia simu kwa matumizi yake binafsi katika kipindi chake chote pamoja na kua alikuwa akiendelea na masomo.
Mnamo mwaka 1922 Alexender Graham Bell alifariki dunia.