Mitandao ya kijamii usitumike kudhalilisha wanawake




JAMII ipatiwe elimu juu ya mitandao ya kijamii,ili mitandao hiyo usitumike kwa kuwadhalilisha wanawake kwa masuala ya ukatili wa kijinsia.

Hayo yalisemwa na Mkurugenzi mtendaji wa TGNP Mtandao,Liliani Lihundi katika mada iliyozungumziwa matumizi sahihi ya mitandao ya kijamii  katika kuchochea usawa wa kijinsia.

Mada hiyo iliyotolewa katika Semina za Jinsia na Maendeleo(GDSS),Lihundi  alisema kuwa  ,ili kukomesha  matukio ya ukatili katika mitandao ya kijamii  inatakiwa elimu itolewe kwa jamii.

" Mtandao ya kijamii ni maisha ya twasira ,kama hakutakuwa na elimu ya kutosha kwa jamii suala la matumizi mabaya ya mitandao litazidi kuendelea," alisema.

Alisema kuwa baadhi ya watu wamekuwa wakitumia mitandao hiyo kuwadhalilisha wanawake.

Zuwena Mweru ambaye ni mkuu wa kitengo  cha ushirikishaji wa jamii kutoka Jamii forum alisema kuwa, mitandao ya kijamii imefanya dunia kuwa kijiji kutokana na taarifa kupatikana kutoka kwa jamii.

Aliongeza kuwa mitandao ya kijamii sio mibaya ,Ila inategemea mtu anaitumiaje.

Alisema zaidi ya watu milioni  4.5 wanatumia mitandao ya kijamii duniani.

" Wanawake ni wachache zaidi katika matumizi ya mitandao ya kijamii kuliko wanaume," alisema.

Aliongeza kuwa kutokuwa na elimu kwa baadhi ya wanawake hali hiyo imewafanya wanawake kushindwa kutumia mitandao ya kijamii.

 Alisema  wanawake wanapenda baadhi ya maudhui katika mitandao hiyo .

Aliongeza kuwa Jamii forum  ilig ,huku wanaume wakipenda zaidi katika mitandao hiyo masuala ya mipira.

Alisema ukatili wa kijinsia katika mitandao ya kijamii Ni pamoja na lugha chafu ikiwamo na kutoa picha za wanawake bira ridhaa yao.

Salome Lubeni ambaye ni mwenyekiti wa kikundi Cha wanawake Mashujaa Machimbo  kata ya Kipunguni Jijini Dar es Salaam alisema kuwa  baadhi ya watu wanatumia mitandao ya kijamii kudhalilisha wanawake.

Alisema kitu ambacho kinatakiwa kufanyika ni kutolewa kwa elimu juu ya matumizi ya mitandao.

Aliongeza kuwa mitandao ikitumiwa vizuri inafaida zake hata kuuza uchumi,lakini Mtandao huo ukitumika vibaya unaleta madhala kwa yule aliyedhalikishwa.

 " Mitandao inafaida na pia inamadhara kutokana na kitu ulichokituma kwa jamii," alisema.

Alisema wazazi wasiwaachie watoto mitandao kuitumia pasipo na faida yoyote.

Alisema elimu kwa jamii izidi kutolewa,kila shule kuanzishwe klabu za kupinga ukatili.

Alisema sheria zichukue mkondo wanaoitumia mitandao vibaya ya kijamii wachukuliwe hatua Kali za kisheria
Tags

Post a Comment

0 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.

Top Post Ad

Below Post Ad