Uchunguzi uliyofanywa na Polisi umebaini kuwa Hamza Mohammed ambaye aliuawa Agosti 25, 2021 baada ya kuua watu wanne alikuwa gaidi wa kujitoa muhanga
Mkurugenzi wa Upelelezi wa Makosa ya Jinai (DCI), Camillius Wambura amesema Hamza alikuwa akiishi kisiri huku akijifunza mambo ya kigaidi kwa kuangalia Mitandao inaoonesha matendo ya Al-Shaabab na makundi kama ISIS
Kwa mujibu wa DCI Wambura, kitendo cha Hamza kilikuwa ni kitendo cha ugaidi wa kujitoa muhanga. Pia, amesema Hamza hakuwa na madini wala fedha katika mazingira yake, akikanusha madai aliwashambulia Askari kwasababu walimdhulumu