Mkuu wa jeshi Marekani asema vita vya Afghanistan vilifeli




Mkuu wa jeshi la Marekani amevitaja vita vya miaka 20 vya nchi hiyo Afghanistan kama vilivyofeli. Jenerali Mark Milley amekiri pia kuwa yeye alipendelea baadhi ya vikosi visalie nchini humo ili kuzuia kusambaratika kwa serikali ya Afghanistan iliyokuwa inaungwa mkono na Marekani na Taliban kuchukua mamlaka kwa haraka.
 
 Milley amesema kwa sasa Marekani inakabiliwa na kitisho kikubwa cha ugaidi."Magaidi wa Al-Qaeda au IS waliojikusanya tena wakiwa na nia ya kuishambulia Marekani, ni jambo linalowezekana kwa sasa.
 
 Na huenda hilo likafanyika katika kipindi cha miezi 12 au 36 ijayo ukizingatia wako sehemu ambayo haina uongozi kwa sasa. Kuwakabili ni jambo gumu kwa sasa ila haimaanishi kwamba haliwezekani. 
 
Na tutaendelea kuwalinda Wamarekani."Milley lakini alikataa kusema ni ushauri gani aliompa Biden mwezi uliopita alipokuwa anafikiria kutekeleza makubaliano ya Taliban na utawala wa Trump wa kupunguza vikosi vya marekani Afghanistan. 
 
Maseneta wa chama cha Republican katika Kamati ya Huduma za Kijeshi hapo jana walisema ushahidi wa jenerali Milley unatosha kuonyesha kwamba Rais Joe Biden hakuwa mkweli katika mahojiano ya televisheni mwezi uliopita aliposema jeshi halikumshauri abakishe vikosi nchini Afghanistan.
 
Tags

Post a Comment

0 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.

Top Post Ad

Below Post Ad