WATU wawili ambao majina yao hayajajulikana mara moja, mwanamke anayekadiliwa kuwa na umri kati ya miaka 25-30 na mtoto wa kiume anaekadiriwa kuwa na umri wa miaka 5-8 wamekutwa wamekufa maji ndani ya Bwawa la Mindu Manispaa ya Morogoro.
Afisa wa Jeshi la Zimamoto na Uokoaji Mkoa Morogoro, Fadhili Makala amesema majira ya saa 12:00 asubuhi Jeshi hilo lilipokea taarifa kutoka kwa mwenyekiti wa Mtaa wa Mindu kuhusu kuonekana kwa miili ya watu hao ndipo walipofika katika bwawa hilo na kuiopoa.
Mkurugenzi Bodi ya Maji Bonde la Wami Ruvu, Mhandisi Elibariki Mmassu amesema watu hao huenda walikua wakifanya shuguli za kibinadamu katika bonde hilo.
Bodi hiyo ilipiga marufuku shughuli zote za kibindamu kutokana na Bwawa hilo kuwa ndiyo chanzo kikubwa cha maji Mjini Morogoro ambapo zaidi ya asilimia 75 ya wanatumia maji hayo.