Msanii Mpya wa Rayvanny Kuja Kuwa Kiboko ya Ibrah wa Konde Gang



Wote ni mafundi wa muziki, binafsi sina shaka na uwezo wa @macvoice_tz kwasababu nimebahatika kumsikia hata kabla ya kusainiwa NLM. Wapo baadhi ya Mashabiki wanaodai ni kiboko ya @ibraah_tz , kwa upande wangu naona si kweli na ni mapema sana kuwashindanisha, Ibrah ni Ibrah, same to Mac Voice.

Shaka nilionayo ni kuwa, Ukimsikiliza Mac Voice aliyeimba “Mama Jay” na @chegechigunda ,si huyu aliyeimba “NENDA” sababu upande huu amekuwa ni Rayvanny wa pili, Tofauti na Ibrah alipokuwa anatoka na wimbo wake wa kwanza kabisa “Nimekubali” hakusound kama @harmonize_tz wa pili hata kwa projects zilizofwata. Hivyo hawezi kuwa kiboko ya Ibra akiendelea kusound kama Rayvanny, maana kutakuwa hakuna la ziada.

Ukiachilia sauti nzuri aliyonayo, lakini pia Mac Voice ana ngoma kali tokea zamani kama Bamba,Teamo na Mama J. Na hata ngoma zote alizotoa kwenye EP yake hii leo ni kali, kikubwa ni kujitafuta awe Mac kama Mac, kuanzia sauti na Melodies (kujitofautisha na Ray) .By the way ni mwanzo mzuri👏

NB: Hizi ni hisia zangu, na ushindani sio uadui bali kunachangamsha game.


Post a Comment

0 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.

Top Post Ad

Below Post Ad