MAMLAKA ya Vitambulisho vya Taifa (Nida) imetoa vitambulisho vya uraia milioni 9.4 tangu ianze kuzalisha vitambulisho hivyo huku vitambulisho 1.3 havijachukuliwa.
Msemaji wa serikali Gerson Msigwa amewataka wananchi kwenda kwenye vituo vyao kuchukua vitambulisho vyao kwa ambao bado hawajafanya hivyo.
“Mkachukue vitambulisho vyenu mlipokwenda kujisajili. Vipo baadhi vilikuja katika ofisi lakini walivibadilisha kwa sababu walitoa taarifa visivyo, hawa mchakato wa kubadilisha unachukua muda lazima mamlaka ijiridhishe isije ikawa ni nia ovu ama anachukua taarifa za mtu mwimwingine,” amesema.
Amesema pia tayari kwamba tayari vitambulisho milioni 8.5 vimeshahakikiwa na kupelkewa kwa wahusika katika vituo mbalimbali.
“Uhakiki unaangalia kitambulisho kimoja kimoja, unaangalia kama jina limekaa sawa na taarifa zote zilizopo kwenye kitambulisho,”amesema.
Amesema watanzania milioni 7.2 wamechukua vitambulisho vyao huku milioni 1.3 vikiwa bado katika ofisini walizoombea.