Mtuhumiwa Kesi ya Mbowe Adai Kufungwa Kitambaa Cheuzi Usoni





MAPYA yameibuka wakati mtuhumiwa namba mbili wa kesi 16/2021, Adam Kasekwa ambaye ni shahidi namba moja katika kesi ndogo ndani ya kesi ya msingi inayomkabili yeye pamoja na wenzake watatu akiendelea kujitetea  mahakama imerejea maelezo ya awali yaliyotolewa mahakamani hapo Septemba 10, mwaka huu yaliyoonesha kuwa Kasekwa alifukuzwa kazi kwa sababu za kinidhamu.

 

Hayo yamejiri leo Jumatatu, Septemba 27, 2021 katika Mahakama Kuu Division ya Uhujumu Uchumi na Rushwa wakati kesi inayomkabili Mwamba Freeman Mbowe na wenzake watatu ilipokuwa ikiendelea mahakamani hapo.

 

Mahakama imeelezwa kuwa maelezo hayo yanakinzana na maelezo aliyoyatoa mahakamani hapa siku ya Ijumaa ya Septemba 24, 2021 aliposema kuwa yeye aliachishwa kazi kwa sababu za kiafya, alipopewa nafasi yakutolea ufafanuzi maelezo hayo yaliyokinzana, Kasekwa alisema hawezi kuyajibia.

 

Aidha, shahidi Ling’wenya ameieleza mahakama namna ambavyo alishuhudia tukio la ukamatwaji wa mshtakiwa namba mbili ambaye ni Adam Kasekwa na kudai kuwa katika tukio hilo mshtakiwa Kasekwa alipigwa kabla yakupelekwa katika kituo cha polisi.

 

Mshtakiwa namba tatu ambaye ni Mohamed Abdillah Ling’wenya ametoa udhahidi ndani ya kesi kutokana na jina lake kutajwa na shahidi namba moja ambaye ni mshtakiwa namba mbili, Adam Kasekwa.

 

Ling’wenya ambaye ameanza kutoa ushahidi wake leo katika kesi ndogo ndani ya Kesi ya Msingi inayomkabili yeye pamoja na wenzake amesema akiwa jijini Dar es Salaam mara baada yakufikishwa Katika kituo cha Polisi Mbweni alibadilishwa jina nakuitwa Johnson John.

 

Kesi hiyo imeahirishwa mpaka kesho saa 3 asubuhi ambapo shahidi wa pili upande wa utetezi ataendelea kutoa ushahidi wake katika shauri dogo la kesi ya msingi.
Tags

Post a Comment

0 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.

Top Post Ad

Below Post Ad