Mvua yasitisha kwa muda Kesi ya Ugaidi ya Mbowe na wenzake




Jaji Mustapha Siyani  anayesikiliza kesi ya ugaidi inayomkabili Mwenyekiti wa CHADEMA Freeman Mbowe na wenzake watatu amesitisha kwa muda kusikiliza ushahidi wa shahidi watatu upande wa utetezi wa shauri dogo  katika kesi ya msingi ya Uhujumu Uchumi kutokana na kukosekana  kwa usikivu mzuri unaosababishwa na mvua inayonyesha.

Leo mapema shahidi wa tatu upande wa utetezi katika kesi ndogo ndani ya kesi ya msingi ya uhujumu uchumi inayomkabili Mwenyekiti wa CHADEMA Freeman Mbowe na wenzake watatu alianza kutoa ushahidi wake katika Mahakama Kuu Divisheni ya Rushwa na Uhujumu Uchumi.
Tags

Post a Comment

0 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.

Top Post Ad

Below Post Ad