Mwanafunzi wa Shule ya Sekondari Nyehunge iliyopo Wilayani Sengerema, Lucas Moshi anashikiliwa na Jeshi la Polisi kwa tuhuma za kuchoma Mabweni mawili ya Shule hiyo Septemba 27
Mkuu wa Wilaya ya Sengerema, Sanyi Ganga amesema Mwanafunzi huyo alisimamishwa masomo na kutakiwa kufika Shuleni na Wazazi lakini hakufanya hivyo, badala yake alikuwa akizunguka maeneo ya Shule
Hakuna Mwanafunzi aliyejeruhiwa wala kupoteza maisha, mbali na mali za Wanafunzi zilizoteketea kwa Moto zikiwemo Nguo, Madaftari pamoja na Magodoro.