Mwanamuziki wa Marekani Rapper Meek Mill Adai Kuponeshwa Tumbo na Dawa za Mitishamba Kutoka Africa


#SNSEnt: Ikiwa tunaisubiri album mpya ya tano kutoka kwa rapper @meekmill ambayo ametangaza kuiachia Oktoba 1, mwaka huu, mkali huyo mzaliwa wa Philadelphia nchini Marekani ameweka wazi kuwa amepona tatizo lake la tumbo kwa mitishamba kutoka Afrika kama miujiza.

#MeekMill amebainisha hayo kupitia ukurasa wake wa twitter akieleza kuwa, tatizo lake hilo la tumbo limekuwa likimsumbua kwa takribani miaka miwili, na ashakutana na madaktari mbalimbali lakini hakupata uafadhali, ila dawa zilizoponesha tatizo hilo ni mitishamba kutoka Afrika.

"Ni takribani miaka miwili nimekuwa nikisumbuliwa na tatizo la tumbo. Nimejaribu madaktari mbalimbali lakini sikupona. Nimetumia mitishamba kutoka Afrika na tumbo langu limepona kama miujiza" ame-tweet Meek Mill.

Post a Comment

0 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.

Top Post Ad

Below Post Ad