Kipaji kutoka mji uliyokosa Maji ya Bluu yani Morogoro, @belle9tz kupitia kipindi cha HOMA ya TV E kilichoruka live jana tarehe 17/9 ametuupdate kuwa mtu wa kwanza kumfungulia njia ya muziki kwa ukubwa zaidi ni mtangazaji wa EFM @bdozen wakati huo akiwa mjengoni CLOUDS MEDIA GROUP.
Kipaji hiki noma cha R&B kilianza kusikika rasmi kwenye masikio ya Watu wengi nchini mnamo mwaka 2009 alipotoa hit song inayoitwa “Sumu ya Penzi” ambayo ilimpa umaarufu mkubwa kabla ya kuja kushindilia na hits nyingine kibao kama "Masogange” na “We ni Wangu” mwaka 2010 na wakati huo mchuano mkali ulikuwa ni kati yake na msanii @diamondplatnumz ambao wote kwa wakati huo walikuwa vijana wadogo na maunderground kwenye game ya Bongo Flava.
Enzi hizo Radio Free Afrika ilikuwa na kipindi kilichoitwa MPAMBANO WA WASANII na wasikilizaji ndio waliokuwa wakipiga kura kwa kupiga Simu, walipopambanishwa mara ya kwanza ngoma ilitoka droo, ikabidi pambano lirudiwe na mara ya pili Belle 9 akamchakaza Diamond kwa kura nyingi sana. Na hata kwenye matamasha kadhaa ya Fiesta Belle 9 alionekana kuwa kivutio cha wengi hasa wadada wakisubiri kumuona Mr. Baby Face, hata pale Diamond alipobeba tuzo 3 za Kili Music Award mbele ya namba 9 bado 9 alisimama kama mpinzani mkubwa wa Diamond.
Maisha yapo kasi sana,hakukuwa na Gap kubwa wakati Belle 9 yupo juu ya Mondy ila kumekuwa na Gap kubwa wakati Diamond yupo juu.Kilichokuja kutokea mtoto wa Tandale akachanganya na ile asili ya watu wa kigoma kuwa ni wabishi wasiokubali kirahisi akikesha studio na baadae kumpindua Belle 9 na hadi leo kamuacha mbali sana.
Mbanga na vurugu zote hizi Belle 9 kafanya ila mwanzoni mwa safari yake, Mtangazaji B Dozen anahusika.
Much Love kwa Twangala kwa kutuletea dhahabu hii kwenye game yetu ya Bongo Flava.