Nabi, Kaze Wabadilishana Mbinu Usiku Simba Afe






LICHA ya kutua usiku wa kuamkia jana, aliyewahi kuwa kocha mkuu wa Yanga, Cedric Kaze, hakutaka kupumzika na akaenda moja kwa moja kambini kukutana na kocha Nasreddine Nabi.

 

Kaze ambaye amerejea kwenye timu hiyo kuja kuwa msaidizi, alilazimika kwenda Avic Town Kigamboni kukutana na Nabi na kufanya kikao, ajenda ikiwa ni kuijadili Simba.

 

Mmoja wa viongozi kutoka ndani ya Yanga aliliambia Championi Ijumaa kuwa, Kaze alitambua umuhimu wa mchezo wa Jumamosi na Simba hivyo aliamua kwenda kukutana na kocha ili kujua wapi amefikia na yeye kuweka mchango wake.

 

“Kweli Kaze alikuja hapa kambini usiku sana, hakutaka kupumzika alikuja kukutana na Kaze na kubwa zaidi walilojadili ni kuelekea kwenye mechi yetu na Simba.

 

“Kikao chao kilikuwa kizito kidogo kwa sababu walitumia muda mwingi kidogo wakizungumza nini wanatakiwa kufanya mbele ya Simba ili waweze kushinda,” alisema mtu huyo.

 

Kwa upande wa Mkuu wa Idara ya Habari na Mawasiliano wa Yanga, Hassan Bumbuli, alisema: “Kimsingi sisi tumeshamaliza kila kitu kwenye mambo ya maandalizi yetu. Hivyo lolote hatuna presha, timu yetu na benchi la ufundi limetimia sana.”

Ibrahim Mussa, Dar es Salaam

Post a Comment

0 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.

Top Post Ad

Below Post Ad