Nabi Mambo Magumu Yanga





IMEELEZWA kuwa Kocha Mkuu wa Yanga, Nasreddine Nabi raia wa Tunisia amepewa mechi mbili ikiwa ataboronga safari itamkuta.

Nabi kibarua chake kimeanza kuwa katika wakati mgumu baada ya kushindwa kufanya vizuri katika mechi mbili za hivi karibuni baada ya Ligi Kuu Bara kumeguka kwa msimu wa 2020/21 na sasa ni muda wa maandalizi ya msimu mpya.

Ilikuwa ni ile ya Wiki ya Mwananchi ambapo ubao wa Uwanja wa Mkapa ulisoma Yanga 1-2 Zanaco siku hii ilikuwa ni rasmi ya utambulisho wa kikosi kazi cha Yanga kwa msimu wa 2021/22.

Pia mchezo wa pili ilikuwa ni ule wa Ligi ya Mabingwa Afrika hatua ya awali ambapo Uwanja wa Mkapa ubao ulisoma Yanga 0-1 Rivers United.

Awali Nabi aliweka wazi kuwa anahitaji muda ili kukiimarisha kikosi hicho kwa kuwa hakupata muda mzuri wa kuwaunganisha wachezaji wake kutokana na kambi ya Morocco kutokuwa kwenye  mpangilio mzuri.

Mechi ambazo inaelezwa kuwa amepewa ni ile ya marudio itakayochezwa nchini Nigeria pamoja na ile ya Ngao ya Jamii dhidi ya Simba, Uwanja wa Mkapa Septemba 25.
Tags

Post a Comment

0 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.

Top Post Ad

Below Post Ad