Mimi nitakuwa Mtu wa mwisho kuamini kuwa Yanga watakuwa na msimu mbaya sana, nitakuwa wa mwisho pia kuamini kuwa Yanga itapata matokeo mazuri mapema hii
Well ofcourse! Kwenye Football yetu ya Afrika haswa Kusini mwa jangwa la Sahara, sehemu ambayo football sio biashara kubwa kuna vitu vitatu, Yanga wanisikilize vyema tu
Kuna kitu kinaitwa GRB MODEL! Yes this is the model! G for Growth (Ukuaji), R for Result Oriented (Matokeo na Mataji) and B for Business (Biashara) hivi ndio vitu vitatu muhimu kwa huu ukanda wetu
Hoja yangu ni nini? Yanga wapo wapi?
Well hoja yangu ni kuwa Yanga kwasasa wapo kwenye GROWTH yani Ukuaji! Yanga si wamesajili? Wamesajili wachezaji watakaoikuza timu, haswa wenye uzoefu
Wazoefu ni kama hao wakina Heritier Makambo, Djuma Shaban, Jesus Moloko, Yannick Bangala, Djigui Diarra na wengine ambao ni push to start, kisha wachezaji Yoso kama Yusuph Athuman na wengine watakua kupitia timu
Hii ndio hatua waliopo kwenye GRB MODEL, na ndipo hapa watapitia magumu kidogo kwakuwa timu unajitafuta ili iende hatua inayofuata!
Kwenye hii hatua ya GROWTH nini kinapaswa kufanywa ila hakifanyiki? Hapa kuna shida ya KIUTAWALA! Yes kinachofanya Yanga wasiondoke hapa mapema ni Hiyo, ni kama wanataka kuivuka hii hatua lakini ni muhimu sana
Manchester United hawapo na Ole kwa bahati mbaya licha ya matokeo mabovu, Liverpool hawakuwa na Klopp kwa bahati mbaya na hata wale Simba wakati Sven anashinda kwa mbinde hawakubaki nae kwa bahati mbaya
Umesema shida ya Yanga ni KIUTAWALA? Yes! Hapo kuna shida, hawajaikubali hii hatua, wanataka shortcut na hii inazalisha presha kubwa kwa Wachezaji!
Nini kifanyike? Watawala waufuate mfumo wa Yanga na sio Yanga watoke kuufuata mfumo wao! Wataipoteza
Nataka nielezee GRB MODEL kama darasa kwa Yanga kupitia SIMBA maana wamefanikiwa sana, naomba andiko lijalo niwaambie kitu kuhusu SIMBA kwenye model hii! NITAREJEA
#jr_farhanjr