IMERIPOTIWA kuwa aliyekuwa mchezaji wa Arsenal, Mesut Ozil hana furaha na timu yake mpya ya Fenerbache ikiwa ni miezi nane pekee imepita tangu kujiunga na miamba hiyo ya Uturuki.
Ozil mwenye umri wa miaka 32, alitua Istanbul mwezi Januari kwa uamisho huru baada ya kufikia makubaliano na Arsenal wakati alipokuwa amesaliwa na miezi sita ya mkataba The Gunners.
Kwa mujibu wa Diario AS, mchezaji huyo ameweka wazi kuhama licha ya kuwa na miaka mitatu ya kandarasi na Fenerbache. Miamba hiyo ya soka nchini Uturuki imeshindwa kuonesha mapenzi naye baada ya kuhusishwa na kutimkia Qatar na MLS.
Baada ya kujiunga na klabu mwezi Januari alishiriki jumla ya michezo 10 baada ya kusumbuliwa na majeraha ya ‘ankle’. Mpaka sasa msimu huu ameanza mchezo mmoja.
Inasemekana Kocha wa Fenerbache, Vitor Pereira hana imani ya kutosha na Ozil na hivyo anapendelea zaidi kumpanga kinda wa miaka 20, Muhammet Gumuskaya.