2014 ni mwaka ambao ulikuwa na washiriki wawili wa Big Brother Africa ambao baadae walikuja kuwa kwenye uhusiano na Madam wemasepetu katika nyakati tofauti.
Alianza @luismunana raia wa Namibia ambaye 2015 alijikuta kwenye huba Zito na Miss Tanzania, Wema Sepetu wawili hao wakikutana kwenye Instagram Party.
Kwenye Moja ya Interview, Wema aliwahi dai kuwa Luis Munana alikuja kwenye maisha yake kipindi ambacho Wema alikuwa anahitaji Faraja, ilikuwa ni muda mchache toka Wema abwagane na msanii @diamondplatnumz . japo hakukuwa na maelezo ya Kutosha ila inaaminika wawili hawa walifunga hadi ndoa. Hii ni baada ya Mnamibia huyo kuweka picha zilizo ashiria uwepo wa jambo hilo kwenye mtandao wake wa kijamii na baadae kufuta.
Jini mkata kamba akaingia kazini na Penzi hili likafa huku Wema akidai sababu kubwa ni jamaa kushindwa kuhandle mahusiano ya mbali. Na baada ya hapo Tanzanian Sweetheart akadondokea kwa mshindi wa big brother Africa 2014, @idrissultan ambaye pia hawakudumu sana,Jini mkata kamba akafanya yake.
Jana September 28,ilikuwa ni Birthday ya Wema Sepetu, na Luis Munana akashea moja ya picha waliowahi kupiga na Wema kisha kuiandikia caption akimtakia kheri ya siku ya kuzaliwa ya miss world wake. Huku wema akijibu kuwa Munana ni mtu pekee aliyevaa viatu vya mzee Sepetu,hivyo bado ni wa kwake hadi leo. Pia Madam hakuishia hapo tu alizama hadi Insta story na kuandika hajui amfanye nini Munana maana anahisi kubarikiwa kuwa na mtu huyo maishani. Wawili hawa wamekuwa wakimisiana sana maana hata Wema aliwahi post instagram akidai anammis mwana hatari.