Wabunge watatu wa Chama cha Mapinduzi (CCM) akiwamo Mbunge wa Kuteuliwa, Humpherey Polepole watawekwa kikaangoni leo na Kamati ya Maadili ya Wabunge wa CCM kuhojiwa kuhusu masuala tofauti.
Wabunge wengine watakaohojiwa leo ni Askofu Josephat Gwajima (Kawe) na Jerry Silaa (Ukonga) ambao Bunge lilipitisha azimio la kuwasimamisha kwa mikutano miwili kutokana na tuhuma za kusema uongo, kushusha hadhi na heshima ya Bunge.
Vilevile, Kamati imependekeza Askofu Gwajima kufikishwa mbele ya kamati ya chama chake CCM na kuhojiwa kuhusu mwenendo wake.
Kamati ya Haki, Maadili na Madaraka ya Bunge ilipendekeza Silaa asimamishwe mikutano miwili ya Bunge la Tanzania na avuliwe uwakilishi kwenye Bunge la Afrika (PAP) kwa madai kuwa anaweza kusema uongo akienda huko.
Kilichomponza Silaa ni kauli yake ya kutaka wabunge wakatwe kodi kwenye mapato yao, jambo lililoelezwa kuwa ni uongo, kwani wabunge wanalipa kodi.
Kwa upande wa Gwajima, atatakiwa kujieleza kuhusu kauli anazozitoa katika Kanisa lake la Ufufuo na Uzima kuanzia Julai 25 mpaka Agosti 15 kuhusu chanjo ya korona.
Akizungumza na gazeti hili jana, Katibu wa Wabunge wa CCM, Rashid Shangazi alisema wametekeleza mapendekezo ya wabunge, akiwamo Spika wa Bunge, Job Ndugai