Maafisa wa polisi kwa mara nyingine wameonywa dhidi ya kuweka vizuizi vyovyote vya barabarani mahali popote bila idhini rasmi.
Pia hakuna gari linalopaswa kuzuiliwa barabarani kwa muda mrefu bila maelezo.
Hatua hiyo mpya imechukuliwa baada ya mkutano kati ya Inspekta Jenerali wa polisi Hilary Mutyambai naibu wake Edward Mbugua, makamanda wa maeneo na makamanda wa kaunti jijini Nairobi.
Mawasiliano kutoka Mbugua yalisema mkutano huo ulibaini kuna vizuizi vya barabarani vinavyozidi kuwekwa barabarani bila idhini licha kinyume na mwongozo uliotolewa hapo awali .
Alimwambia kila kamanda kuhakikisha kuwa hakuna vizuizi vya barabarani, ukaguzi wa trafiki, hakuna kuiziliwa magari kando ya barabara kwa muda mrefu na hakuna kuchukua rushwa kutoka kwa waendeshaji magari ndani ya sehemu wanazosimamia