Polisi watuhumiwa kushika sehemu za siri za wanawake kinguvu




Jeshi la Polisi Wilayani Handeni Tanga limelalamikiwa kwa vitendo vya unyanyasaji vinavyofanywa na baadhi ya Askari wake kwa kuwalazimisha mapenzi Wanawake na kuwashika sehemu zao za siri bila ridhaa yao wakiwa maeneo ya starehe na sehemu nyingine.

Wakiongea kwenye mkutano wa hadhara ulioitishwa na Kamati ya Ulinzi na Usalama Wilaya ya Handeni chini ya Mwenyekiti wake ambae ni Mkuu wa Wilaya hiyo Sirieli Mchembe, Wanachi pamoja na Wananchi wengine wamepaza sauti kusema unyanyasaji ambao umekua ukifanywa na baadhi ya Askari Polisi.

Mmoja wa Wanawake hao wamesema "Kuna Askari wakija humu ndani 'night club' wanatushika bila ridhaa yetu.. wanataka Wanawake kilazima, akiona Mwanamke anamkataa anamtafutia sababu anamkamata kwenda kumlaza sero"

Mmoja wa Wanawake hao wamesema "Kuna Askari wakija humu ndani 'night club' wanatushika bila ridhaa yetu.. wanataka Wanawake kilazima, akiona Mwanamke anamkataa anamtafutia sababu anamkamata kwenda kumlaza sero"

Mmoja wa Vijana wa kiume waliosimama kuongea amesema "Wakija humu ndani wanatufanyia jinsi wanavyotaka wao, Demu wako mzuri anachukuliwa ukizingua unapigwa"

Mwananchi mwigine aliesimama alisema "Anakuja na bunduki anaingia ndani mpaka Club humo ndani anachukua Mtoto wa kike anafanya vile anavyotaka, hata mimi siku hiyo nilikua natoka safari roho iliniuma na ukiangalia gari ya Polisi imepaki pale, anafanya unyama"

Baada ya Malalamiko hayo ya Wananchi Mkuu wa Wilaya Sirieli Mchembe alitoa tamko la Serikali huku akielezea tukio la hivi karibuni la Mabinti wawili kupigwa na Askari hao ndani ya moja ya kumbi za starehe zilizopo Wilayani Handeni jambo lililopelekea kuitisha mkutano nje ya ukumbi huo huku kura za siri zikipigwa kuwataja Askari hao.

"Hakuna Askari mwenye mamlaka ya kumgusa au kumchezea Mwanamke maeneo yake bila kibali chake, cheo cha Mtu hakihusiani na mwili wa Mtu, Mabinti wale watakuja hapa mtaona mmoja mpaka sasa hivi jicho limevimba wamepigwa mangumi ya hatari, Mimi kama DC Mwanamke unyanyasaji wa kijinsia Handeni hapana" Mkuu wa Wilaya Handeni Sirieli Mchembe.

Post a Comment

0 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.

Top Post Ad

Below Post Ad