R. Kelly alimnyanyasa kingono mwimbaji wa zamani wa R&B marehemu Aaliyah wakati alipokuwa na umri wa miaka 13 au 14, mmoja wa wacheza densi wake wa zamani ameiambia korti.
Mwanamke huyo, ambaye alitoa ushahidi chini ya jina Angela, aliiambia korti kwamba alikuwa ameona nyota huyo akifanya tendo la ngono kwa Aaliyah kwenye basi la usafiri
Tukio hilo linadaiwa kutokea mwaka mmoja kabla ya Bwana Kelly kuoa mwimbaji huyo kinyume cha sheria, akiwa na miaka 15.
Bwana Kelly, 54, anakanusha mashtaka yote dhidi yake.
Ni pamoja na shtaka moja la udanganyifu - ambalo linamtaja kama mkuu kundi lenye hila la "kuwateka wasichana na vijana" kwa malengo ya ngono’. Ameshtakiwa pia kwa mashtaka manane ya kukiuka sheria za kuzuia ngono kati ya majimbo.
Mwimbaji huyo, ambaye jina lake kamili ni Robert Kelly, hakushtakiwa kwa kubaka au kushambulia, lakini waendesha mashtaka wanaruhusiwa kutoa ushahidi wa uhalifu unaowezekana unaohusiana na mashtaka ya ujambazi, bila kujali ni lini yalitokea.
Ushuhuda wa Angela ulikuja siku ya 15 ya kesi, huko Brooklyn, New York.
Alikuwa mtu wa 10 anayetuhumu R Kelly kusimama kortini kutoa ushahidi na akasimulia kisa cha unyanyasaji wa kijinsia wa waathiriwa waliokuwa na umri mdogo .
Alisema alianza kufanya mapenzi na Bwana Kelly mnamo 1991, wakati bado alikuwa shuleni.
Kesi hiyo inaendelea