KESI ya mwimbaji wa R&B nchini Marekani R. Kelly mapema wiki hii imeanza kuunguruma katika mahakama huko Brooklyn, New York. Inaripoti Mitandao ya Kimaita … (endelea).
Nyota huyo anayetuhumiwa kwa ulaghai, unyanyasaji wa kijinsia na rushwa ya ngono, licha ya kukanusha mashtaka hayo mara kwa mara, mwanamke mwingine amejitokeza kumkaanga.
Baadhi ya madai yaliyotolewa dhidi ya mwimbaji huyo ambaye jina lake kamili ni Robert Sylvester Kelly – yameanza zaidi ya miaka 20.
Shahidi wa kwanza, Jerhonda Johnson Pace aliwaambia majaji kuwa R. Kelly alijua kwamba ana umri chini ya miaka 17 iliyodhinishwa walipofanya ngono huko Chicago mwaka 2009.
Pace ambaye sasa ana miaka 28 pamoja na watoto wanne kwa mwanaume mwingine, alipokutana na R. Kelly alikuwa na umri wa miaka 16 lakini awali alimdanganya kuwa na umri wa miaka 19.
“Tulipofanya kitendo hicho… nilikuwa mwenye wasiwasi. Nilihisi kama haikuwa sawa, nikamwambia sijawahi kushiriki ngono, pia nikamwambia ukweli kuhusu umri wangu.
“Aliniuliza,” Hiyo inamaanisha nini? ” na akaniambia… niwaambie watu nilikuwa 19 lakini niigize kuwa nina miaka 21, ” alisema Pace, ambaye anakubali kuwa alikuwa shabiki wa mwimbaji huyo.
Pace aliongeza kuwa katika uhusiano wao uliodumu kwa muda wa miezi sita pekee, alifanikiwa kutoka na tisheti ambayo alikuwa amefutia mbegu za kiume za R. Kelly.
Wakili Msaidizi wa Serikali ya Marekani, Maria Cruz Melendez alisema kuwa katika vipimo vya vinasaba walivyopima kwenye tisheti hiyo vimethibitisha kuwa ni R. Kelly.
Hata hivyo, Wakili wake R. Kelly Nicole Blank Becker alisema mwanamke huyo ni muongo.
Ikiwa R.Kelly mwenye umri wa miaka 54 atakutwa na hatia kwa makosa yote anaweza kuhukumiwa kifungo cha miongo kadhaa gerezani.