Aliposhika kipaza sauti na kuimba "STORM IS OVER" Kila mtu mwili ulikuwa unasisimka na kila mtu huwa alikuwa anaamini hata kama anapitia kwenye magumu basii Kuna muda magumu hayo yangeisha na kila kitu kingekaa sawaa kwenye mahala pakee.
Lakini hata alipokuja pale South Africa wakati wa kombe la dunia mwaka 2014 alikusanya watu na kuimba nao goma Moja kali saana #SIGN OF THE VICTORY" akimaanisha kwamba ilikuwa ni ishara ya ushindi kwa bara la Africa lakini kwako binafsi pia ulikuwa una kila sababu ya kufurahia wimbo huo haswaa pale unapoona ulichokuwa unakipambania unaelekea kwenye mafanikio.
Bahati mbaya saana mwenye kutunga ngoma hizo @rkelly kwake ngoma zake zote zimegoma kufanya kazi kwenye maisha yake "THE STORM IS NOT OVER" and "THERE IS NO SIGN OF THE VICTORY" Kwa Sasa hatima yake iko kwenye kusubiri hukumu ya eidha miaka zaidi ya 10 au kifungo cha maisha kutokana na kukutwa na hatia kwenye makosa yake yote yanayohusisha udhalilishaji wa kingono kwa mabinti chini ya miaka 18.
Leo #KingOfRnB duniani @rkelly amefilisika kiasi kwamba Wikipedia yake inasoma kwamba ana utajiri wa NEGATIVE BIL.4.6 Kwa maana anaishi kwenye madeni kwa Sasa.
Imekuwaje maisha yanaenda kasi kiasi hiki,imekuwaje leo mtu mwenye heshima thamani yake inapotea,imekuwaje maneno yake ya hamasa yameshindwa kumsaidia leo hii analia @rkelly haoni hata rafiki yake mmoja akiwa amesimama upande wake yaani Kama hawamjui vilee.
Tujifunze wakati mwingine makosa yetu wakati tuko kwenye ubora yanaweza kuja kutuhukumu badae bila kutegemea na heshima yote ikapotea.
Anyway niseme tu kwamba ngoma zake bado zitaishi na zitaendelea kubaki kama kumbukumbu kama huko ataweza kuendelea kutupatia burudani tutashukuru Ila mengine tuishie hapa nakusema kama ameonewa basi ipo siku haki yake itasimama na atarudi uraiani.
#KingOfRnB