Rada zaleta neema ya mapato nchini




 
SERIKALI imesema rada nne za kuongozea ndege zilizofungwa katika viwanja vinne vya ndege zimesaidia kuongeza idadi ya ndege zinazotua na kuruka pamoja na mapato yatokanayo na tozo za kutumia anga la Tanzania.

Naibu Waziri wa Ujenzi na Uchukuzi, Mwita Waitara, aliyasema hayo mwishoni mwa wiki jijini hapa alipofanya ziara katika Uwanja wa Ndege wa Mwanza kwa ajili ya kukagua shughuli mbalimbali ikiwamo kuangalia rada ya kuongoza ndege inavyofanya kazi.

Alisema serikali imewekeza fedha nyingi kununua rada hizo ambazo zimefungwa Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Mwalimu Julius Nyerere (JNIA), Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Kilimanjaro (KIA), Songwe na Mwanza na kwamba uwekezaji huo umeanza kuleta matunda.

Kadhalika alisema kwa sasa rada hizo zinasaidia kuona ndege zote zinazopita katika anga la Tanzania na zote zinalipa tozo za serikali.

Aliwapongeza vijana wa kitanzania wanaoongoza rada hizo na kwa sasa nchi inajiongoza yenyewe, badala ya kutegemea wataalamu kutoka nje ya nchi.


 
"Nimeenda Songwe, Dar es Salaam, Kilimanjaro na hapa Mwanza kwa kweli nimeona serikali ilivyofanya uwekezaji katika usafiri wa anga," alisema.

Waitara alisema rada hizo pia zimesaidia ulinzi wa nchi kwa kuwa zinaona kila kitu kinachokatiza katika anga la Tanzania.

Kuhusu mapato, Waitara alisema yamepanda licha ya kuwapo ugonjwa wa Covid-19 katika nchi mbalimbali duniani.


Kwa upande wake, Meneja wa Uwanja wa Ndege wa Mwanza, Pascal Kalumbate, alisema sekta ya utalii kwa sasa imeimarika wanapokea ndege nyingi uwanjani hapo.

Pia kwa sasa ulinzi katika uwanja huo umeimarika kutokana na kufungwa mtambo huo unaofanyakazi saa 24 kwa siku.

Post a Comment

0 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.

Top Post Ad

Below Post Ad