Rais Joe Biden wa Marekani ataadhimisha kumbukumbu ya miaka 20 ya shambulizi la 9/11 kwa kufanya safari za maeneo matatu ambayo mashambulizi hayo yalifanywa.
Kwa mujibu wa Ikulu ya Marekani, Septemba 11, rais huyo na mke wake Jill Biden watatoa heshima na kuwakumbuka waliokufa katika mkasa huo uliotokea miaka 20 iliyopita.
Watashiriki katika shughuli iliyoandaliwa New York, ambapo magorofa mawili pacha ya Kituo cha Kibiashara cha Kimataifa yaliporomoka, kwengine ni Shanksville, Pennsylvania eneo ambalo ndege iliyotekwa na watu wanne wenye itikadi kali ilipata ajali na Arlington, Virginia, ambako wizara ya ulinzi ya Marekani ilishambuliwa.
Biden alipanga kufanikisha maadimisho hayo kwa kuyaondosha majeshi ya Marekani katika vita vya muda mrefu huko Afghanistan hatua ambayo iliitimishwa kwa kuuwawa kwa wanajeshi wa Marekani 13 katika shambulizi la katika uwanja wa ndege wa Kabul