Rais Samia Awapambanisha Ali Kiba na Diamond Platnumz Jukwaani



RAIS Samia Suluhu Hassan anatarajiwa kuwapambanisha manguli wa Bongofleva nchini, Diamond Platnumz na Alikiba ambao imekuwa nadra kukutana kuperfome katika jukwaa moja. Anaripoti Mwanaharusi Abdallah TUDARCo … (endelea).

Tukio hilo la kipekee ambalo limevuta hisia za mashabiki wa wasanii hao ambao wamejengea uhasimu wa kiushindani, wanatarajiwa kushusha mvua ya burudani katika uzinduzi wa Kitabu cha Mkakati wa uelimishaji na uhamasishaji wa sensa ya watu na makazi ya mwaka 2022 jijini Dodoma leo tarehe 14 Septemba, 2021.

Kila msanii kwa wakati wake ameweka tangazo kwenye akaunti yake ya mtandao wa Instagram kuwamasisha wananchi kujitokeza katika tukio hilo.


Alikiba aliandika hivi; “Dodoma, kesho (leo) kuanzia saa mbili asubuhi nitakuwepo Jamhuri Stadium katika uzinduzi wa Mkakati wa Uelemishaji na Uhamasishaji wa Sensa Ya Watu na Makazi 2022.


Wakati Diamondi naye alifunguka hivi; “Hebu muamshe mwenzio alielala hapo mwambie Simba kesho (leo) atakuwepo uwanja wa jamuhuri katika uzinduzi wa mkakati wa Uelimishaji na Uhamasishaji wa Sensa ya watu na Makazi ya 2022!”

Hii ni mara ya pili kwa Kiba na Mondi kukutana katika jukwaa moja jijini Dodoma ambapo mwaka jana hayati Rais John Magufuli aliwakutanisha kwa mara ya kwanza wasanii hao kwenye jukwaa hilohilo la uwanja wa Jamhuri wakati wa kampeni zake za uchaguzi mkuu 2020.


Rais Samia Suluhu Hassan
Aidha, kwa mujibu wa taarifa iliyotolewa na Mkuu wa Dodoma na Mkuu wa Mkoa wa Dodoma, Anthony Mtaka tukio hilo linalenga kuandaa umma na wadau kwa ujumla kwa ujio wa sensa ya watu na makazi ya mwaka ujao.


Amesema uzinduzi huo unaokwenda na kauli mbiu inayosema “Sensa kwa maendeleo, jiandae kuhesabiwa”, utahudhuriwa na viongozi mbalimbali akiwemo Mwenyekiti wa kamati ya Kuu ya sensa, Waziri Mkuu wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Kassim Majaliwa (Mb) na Mwenyekiti mwenza kutoka Zanzibar, Makamu wa pili wa Rais, Hemed Suleiman Abdallah.

Amewataja viongozi wengine kuwa ni Kamisaa wa Sensa Tanzania Bara, Anna Makinda, Kamisaa wa Sensa Zanzibar, Balozi Mohamed Haji Hamza, pamoja na Mawaziri, Manaibu Waziri, Makatibu wakuu, Manaibu katibu wakuu na viongozi wa Serikali kutoka Mikoa minne.

Post a Comment

0 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.

Top Post Ad

Below Post Ad