Rasmi Simba Kuwashusha Al Ahly Simba Day





HII ni ‘next level’ ndivyo unavyoweza kusema ambapo uongozi wa Simba rasmi umethibitisha kufanya mazungumzo na mabingwa wa Afrika, Klabu ya Al Ahly kwa ajili ya kucheza nao katika tamasha la Simba Day Agosti 19, mwaka huu.


Pamoja na burudani ya soka tamasha hilo pia hutumika kuwatambulisha rasmi wachezaji watakaotumiwa na timu hiyo kwa msimu ujao wa 2021/22.


Taarifa kutoka ndani ya Simba zinaeleza kuwa tayari Al Ahly, imepokea mwaliko wa kuja Tanzania kwa ajili ya kushiriki tamasha hilo ambapo, lengo kubwa la michuano hiyo ni kuiandaa timu kwa ajili ya michezo ya kimataifa msimu ujao na kumuaga rasmi aliyekuwa kiungo mshambuliaji wao, Luis Miquissone aliyejiunga na wababe hao wa Misri.


Mwenyekiti wa Simba, Murtaza Mangungu alisema: “Kwa sasa hatuwezi kuweka wazi kuhusiana na uratibu wa tukio letu la Tamasha la Simba kwa kuwa bado tunaendelea na maandalizi, tutaweka wazi kila kitu pale muda utakapokuwa tayari.


“Lakini naloweza kukuthibitishia ni kuwa tutaalika timu moja kubwa kutoka nje ya nchi, tupo kwenye mazungumzo na timu kubwa hapa Afrika kama Al Ahly, Zamalek, Horoya ili kuangalia uwezekano wa wao kupata nafasi ya kuja kwenye tamasha hilo.”

Tags

Post a Comment

0 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.

Top Post Ad

Below Post Ad