RC Makalla asikiliza na kutatua migogoro ya wananchi hadi Usiku Mbagala



Mkuu wa Mkoa wa Dar es salaam Mhe. Amos Makalla amelazimika kusikiliza na kutatua Migogoro ya kila mwananchi aliewasilisha kero yake kwenye mkutano wake Jimbo la Mbagala ili kuhakikisha kila aliewasilisha kero anasikilizwa na kupata ufumbuzi.



Uamuzi wa RC Makalla kusikiliza Migogoro ya Wananchi hadi majira ya usiku ni Kufuatia mwitikio mkubwa wa Wananchi waliowasilisha kero zao.

RC Makalla amefanikiwa kusikiliza na kutatua Mamia ya Migogoro ya Wananchi waliowasilisha ambapo Migogoro iliyoonekana kuhitaji ufuatiliaji wa kina amezikabidhi idara husika kwaaajili ya utatuzi.

Miongoni mwa kero zilizowasilishwa ni Migogoro ya ardhi, Ubovu wa Barabara, Mirathi, Biashara holela, Dhuluma, kero ya Maji na Migogoro mingine.



Aidha RC Makalla ameamuru kuondolewa kwa watu wote wanaofanya biashara ndani ya eneo la Ujenzi wa Barabara ya Mwendokasi eneo la Mbagala Rangi tatu kwakuwa inahatarisha usalama wao na kumzuia Mkandarasi kufanya majukumu yake.

Hata hivyo RC Makalla amezielekeza Taasisi zote zinazomiliki Maeneo Makubwa ya ardhi kuhakikisha wanayalinda na Kuyaendeleza kwakuwa yamekuwa chanzo Cha tatizo la Migogoro ya Uvamizi wa Ardhi.



Mkuu wa Mkoa wa Dar es salaam Mhe. Amos Makalla kesho September 03 ataendelea na ziara yake ya kusikiliza na kutatua Migogoro ya Wananchi wa Jimbo la Kigamboni kuanzia saa mbili Asubuhi Hadi Jioni.

Tags

Post a Comment

0 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.

Top Post Ad

Below Post Ad