Rick RoseyAfunguka Kuhusu Kuwekeza Afrika na Kutembelea Tanzania Kwa Wiki Moja



Msanii wa Hip Hop kutokea nchini Marekani, Rick Ross amesema ana mpango wa kufungua tawi la lebo yake ya Maybach Music Group (MMG) barani Afrika.

Rick Ross amefunguka hayo kwenye Exclusive Interview na Lil Ommy ambapo amesema anapenda sana kushirikiana na wasanii wa Afrika.

Tayari Rick Ross amefanya kolabo na wasanii wa Afrika kama kundi la P Square toka nchini Nigeria ambapo waliachia wimbo 'Beautful Onyinye', na Diamond Platnumz toka Tanzania, ngoma, Kadogo.

Pia kuwa tayari kutumia lugha ya Kiswahili kwenye nyimbo zake, kuwekeza Afrika, Tanzania, kutembelea Serengeti na mlima Kilimanjaro kwa muda wa wiki moja.

Katika interview hii, Rozay The Boss amelezea mambo zaidi ya 10 yatakayokufanya ufanikiwe katika Maisha.

Vile vile ameongelea alivyofanya wimbo na Diamond Platnumz (waka waka, ilikuaje), ukaribu wake na Hamisa Mobetto, Drake, Belaire, Villon pamoja na Biashara zake Wings. Kumiliki magari zaidi ya 100, kununua magari ya zamani, Nyumba yake kutumika kwenye Movie ya Coming 2 America 2 (The Royal Palace).

Rick Ross ameachana pia Grammy, amezungumzia kitabu chake kipya 'The Perfect day to Boss Up' jinsi anavyoamka asubuhi, vitu anavyofanya na kila kitu kuhusu Muziki na Maisha yake!.

Lil Ommy, amemuliza pia kuhusu kumiliki leseni ya gari akiwa ana magari zaidi ya 100 na hakuwa kuwa na leseni!

Amesema Kuwa Atakuja Kutembelea Mlima Kilimanjaro pamoja na Mbuga Ya Serengeti Akikaa Kwa Muda Wa Wiki Moja

Hii Ni Baada Ya Rapa Huyu Kuulizwa na Mtangazaji LilOmmy Kama Hapo Kabla Ameshawahi Kufika Katika Mlima Kilimanjaro Pamoja na Mbuga Ya Wanyama 🇹🇿 Serengeti

"Nimekuwa nikipasikia serengeti kwenye Maisha yangu, lakini mimi mpaka kufika hapa leo kuna miaka 10 ya msoto nyuma, Imefikia muda sasa wa kufurahia maisha na uwezo ninao wa kwenda kutembelea mlima kilimanjaro kwa muda wa wiki moja,

Post a Comment

0 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.

Top Post Ad

Below Post Ad