Ruto akubali kupatanishwa na Uhuru




Naibu Rais wa Kenya William Ruto ameafiki nia ya Maaskofu wa Kanisa Katoliki nchini Kenya ya kumpatanisha na Rais Uhuru Kenyatta, limepoti gazeti la Daily Nation nchini humo.

Katika mazungumzo na viongozi wa kidini wa mashinani nyumbani kwake eneo la Karen Nairobi, Bw Ruto alisema yuko tayari na ana utashi wa kukutana na Rais Kenyatta.

Bwana Ruto alisema uhasama baina yake na rais ulisababishwa na “watu kutoka nje” ambao “walitaka kunufaika na serikali ambayo hawakuiunda .”

“Huwezi kudoea serial ambayo hukuunda,” taliongeza Bw Ruto . Akisema kuwa makubaliano ya Machi 2018 yanayofahamika kama ‘’handshake’’baina ya kiongozi wa chama cha upinzani cha ODM Raila Odinga na Rais Kenyatta yalikuwa chanzo...

“Kuna watu tu wakorawa likuja hapo wakasema huyu deputy president kwanza tuweke kando,” alisema “Lakini mimi niko tayari wakati wowote bila masharti,” limenukuu gazeti la citizen nchini humo

Mzozo baridi umekuwa ukiendelea baina ya kambi ya rais Uhuru Kenyatta na ile ya Naibu rais William Ruto baada ya makubaliano baina ya Rais Kenyatta na kiongozi mkongwe wa upinzani yaliyoitwa ’’Handshake’’.

Upande wa Rais Kenyatta unadai kuwa ‘’handshake’’ ilihusu makubaliano ya kurejesha umoja miongoni mwa Wakenya na hivyo kukomesha ghasia za kikabila zinazoibuka hususan kila baada ya uchaguzi.

Hata hivyo Bw Ruto anadai kuwa hakuhusishwa katika makubaliano hayo, na amekuwa akitengwa na Bw Kenyatta katika masuala mbali mbali ya kitaifa baada ya ‘’Handshake’’

Post a Comment

0 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.

Top Post Ad

Below Post Ad