Saluni ya India yapigwa faini ya $271,000 kwa 'kumnyoa' mteja visivyo








Mahakama ya watumiaji nchini India imeamuru saluni moja kulipa dola 271,000 kufidia hatua ua kumyoa visivyo mwanamke mmoja.

Inasemekana mwanamke huyo alikuwa akipata kazi kutoka makampuni ya bidhaa za nywele kwa sababu ya nywele zake ndefu.

Lakini saluni hiyo ilikata nywele zake fupi kinyume na maagizo yake, na kumsababishia hasara kubwa, mahakama ilisema.

Saluni hiyo, ambayo ni sehemu ya mkusanyiko wa hoteli kadhaa maarufu mjini Delhi, inaruhusiwa kukata rufaa dhidi ya uamuzi huo. Lakini bado haijatoa taarifa juu ya uamuzi huo.

Tume ya Kitaifa ya Kushughulikia Mizozo ya Kibiashara (NCDRC) imesema mwanamitindo huyo amepoteza "kazi aliyokua akisubiri na kupata hasara kubwa ambayo imebadilisha mtindo wake wa maisha kabisa".

Mwanamitindo huyo alikwenda kwenye hoteli mnamo 2018 ili kukata nywele na akatoa maagizo maalum kwa wafanyikazi juu ya muonekano anaotaka.

Lakini msusi wa nywele alikata sehemu kubwa ya nywele zake, "akiacha inchi 4 tu kutoka juu ikigusa bega lake," kulingana na nyaraka za mahakama.

"Aliacha kujiangallia kwenye kioo. Yeye ni mtaalamu wa mawasiliano na [anahitajika] kushiriki katika mikutano na vikao kupitia video. Lakini hajiamini tena kufuatia kisa hicho," amri ya mahakama ilisema.


Post a Comment

0 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.

Top Post Ad

Below Post Ad