Rais wa Tanzania, Samia Suluhu Hassan amesema Kiswahili kimekua kiasi cha kuweza kutumika Kimataifa hali ambayo ilimfanya atake kuongea Kiswahili alipokuwa akihutubia Mkutano wa Baraza Kuu la Umoja wa Mataifa (UNGA)
Akihojiwa na Idhaa ya Kiswahili ya UN, Rais amesema alishindwa kutumia lugha hiyo kwa kuwa katika msafara hawakuwa na Mkalimani na hawakujiandaa kwa hilo, hali iliyomlazimu kutumia Kingereza
Ameongeza kuwa, Kiswahili imekuwa ni lugha ya Biashara kwa Kanda ya Afrika Mashariki na SADC na hata ukienda Ulaya ukimsema mtu kwa Kiswahili ujiangalie maana wanaweza kukujibu kwa Kiswahili