Pole sana ndugu yangu @madeeali tatizo mnaaminishwa sana vitu vya kipumbavu kuliko uhalisia, timu imara ya kushindana inaandaliwa kwa mikakati na siyo blabla, mpira una ABC's zake na lazima ziheshimike, uliwahi kuona wapi tangu dunia inaumbwa timu inawaacha kwa mkupuo magolikipa wake wawili tegemezi?
Lazima tukubaliane vilabu vyetu havina watu sahihi (watalaam) wanaofanya maamuzi, mipango endelevu pamoja na uchumi wa kuviwezesha kusajili wachezaji wenye uwezo wa kuja kuvisaidia kupata matokeo mazuri ya papo kwa papo kama wengi tunavyotaka, matokeo yake tunajikita kusajili wachezaji wenye majina makubwa badala ya kusajili wachezaji bora.