Simba Sc Ashindwa Kufurukuta Mbele ya Biashara United..Bocco Atoa Boko




MABINGWA watetezi wa Ligi Kuu Bara, Simba Sc wamekubali kubanwa mbavu na Wanajeshi wa mpakani, Biashara United baada ya kukubali sare ya bila kufungana katika mchezo wao wa kwanza wa Ligi Kuu msimu huu.


Mechi hiyo imepigwa katika Dimba la Karume mjini Musoma. Simba wamekosa nafasi ya dhahabu dakika za nyongeza baada ya kupata penati ambapo nahodha wao John Bocco amekosa penati hiyo. Simba wanagawana ponti moja moja na Biashara.


Ikumbukwe kuwa hii ni mechi ya tatu mfurulizo kwa Simba bila kupata bao lolote, kuanzia Mechi ya Simba Day waliofungwa bao 1-0 na TP Mazembe, mechi ya Yanga ya Ngao ya Jamii ambapo Simba aliambulia kichapo cha bao 1-0 na game ya leo ambayo wote wameambulia patupu.

Post a Comment

0 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.

Top Post Ad

Below Post Ad