Jamii ya watu weusi nchini Marekani bado imeendelea kuonyesha kuchukizwa na kitendo cha Tuzo kubwa za nchini humo zinazoitwa “Emmy Award” zinazofanyika kila mwaka huku mwaka huu zikifanyika September 19 ikiwa ni mara ya 73 toka kuanzishwa kwake mwaka 1949, baada ya kuingia kwenye headlines tena ambapo categories zote za tuzo hizo kutoa washindi Wazungu tu mwaka huu na Blacks wakiambulia za uso.
Emmy Awards hutolewa na NATIONAL ACADEMY OF TELEVISION ARTS AND SCINCE nchini Marekani, uhusika zaidi na na maudhui ya TV zikiangazia zaidi kwenye documentary film na series kama dramatic series,Comedy series,special drama na limited series ambapo Tuzo utolewa kwa waigizaji,waandishi,waongozaji (Directors) lakini pia wabunifu wa sanaa na na wale technicians.
Mastaa wengi wamezitukana tuzo hizo kuwa zina ubaguzi akiwemo 50 cent na leo hii pia msanii @snoopdogg amepitisha tusi kwenye tuzo hizo huku akidai tuzo hizo hazipo kwaajili ya mtu mweusi na kuziita tuzo za kipumbavu.