Taliban inadai sasa inadhibiti kabisa jimbo la Panjshir la Afghanistan, sehemu ya mwisho kupinga utawala wake.
Kumekuwa na mapigano makali katika eneo hilo kaskazini mwa mji mkuu Kabul, na kundi la (NRF) limekuwa mstari wa mbele kupinga utawala wa Taliban.
"Pamoja na ushindi huu, nchi yetu imeondolewa kabisa kwenye tishio la vita," msemaji wa Taliban alisema.
Hata hivyo , NRF imekana kushindwa na Taliban
"Sio kweli, Taliban hawajadhibiti Panjshir ninakataa madai ya Taliban," msemaji wa NRF Ali Maisam aliambia BBC.
Taliban ilichukua udhibiti wa Afghanistan yote wiki tatu zilizopita, ikichukua mamlaka huko Kabul mnamo Agosti 15 kufuatia kuanguka kwa serikali inayoungwa mkono na nchi za Magharibi.