Timu ya taifa Taifa Stars imetoka sare ya goli 1 - dhidi ya wenyeji DR Congo kwenye mchezo wa kutafuta tiketi ya kufuzu kwa fainali za kombe la Dunia 2022 nchini Qatar.
Wenyeji wa mchezo huo DR Congo walipata bao la kuongoza dakika za mapema 23' kupitia kwa mchezaji wao Mbokani na Tanzania kusawazisha dakika ya 35' kupitia kwa Msuva.
Stars imefanikiwa kupata alama moja mbele ya timu ngumu na bora kabisa barani Afrika.