Tupac Atimiza Miaka 25 Baada ya Kifo Chake, Aliuawa Akiwa na Miaka 25



Kwa wapenzi wa muziki wa magharibi nikimaanisha Marekani wanajua kuwa September 13, 1996 moja ya Rapa bora aliyewahi kutokea kwenye ulimwengu huu Tupac Shakur alifariki baada ya kupigwa risasi takribani nne mwilini mwake na baada ya kulazwa hospital kwa siku 6 kutokana na risasi hizo ambapo alipigwa akiwa kwenye gari moja na aliyekuwa meneja wake Suge Knight ambaye kwa sasa yupo gerezani.



Jina lake la kuzaliwa ni Tupac Amaru Shakur ila wengi wanamfahamu kwa jina la 2Pac au Makaveli, enzi za uhai wake aliwahi kuingia kwenye Guinness World Record kutokana na mauzo ya album yake kutajwa kufikia milioni 74 Dunia nzima lakini milioni 44 kwa mauzo ya Marekani pekee kama msanii wa muziki wa Hip Hop.

2Pac alitamba na ngoma nyingi kali zikiwemo Hit Em Up, Dear Mama, Only God Can Judge Me, Life Goes On na nyingine nyingi aliwahi pia kushiriki kwenye filamu mbalimbali ikiwemo Poetic Justice akiwa na Janet Jackson , Above the Rim, Juice.

Siku ya jana ndio ilitimia miaka 25 tangu kifo cha 2pac Shakur nguli wa Hip Hop duniani sio kutimia tu pia Tupac alipigwa risasi akiwa na miaka 25 .

Kitu cha kukumbukwe kwenye muziki wake ni kwamba hadi hivi leo inakadiriwa kuwa Pac aliuza zaidi ya nakala million 75 ya album zake zote.

Moja ya Interview za Tupac za kukumbukwa ni hii alivyosema. “Everybody rap, we don’t rap, we rap to make money, we do busness… Msanii wa Bongo Fleva chukua hiyo.


Post a Comment

0 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.

Top Post Ad

Below Post Ad