SIMULIZI ya bondia Twaha Kiduku katika gazeti la Championi Jumamosi aliishia kusimulia mipango yake baada ya kuachana na mchezo wa ngumi na kuonyesha nini alichokipata kupitia mchezo huo. Endelea.
“Kikubwa namshukuru Mungu kwa nafasi hii aliyonipa Mungu, nitajitahidi kuitumia vizuri hata kama itakuja kuisha na kuja wengine basi nijue ngumi imenipa nini na nini.
Sasa unampango wowote wa kuanzisha kituo cha vijana kujifunza ngumi?
“ Nilikuwa nao hata kabla sijajulikana maana nilianza kufundisha hata kabla ya kufundishwa maana nilikuwa sijui chochote ila namshukuru Mungu ndiyo nikakutana na mwalimu Pawa Iranda Jeuri ya Tanzania ila GYM ya King Stone bado ipo na mmoja kati ya mabondia wangu walicheza pale.
Jina la Kiduku umelipata vipi?
“Kiukweli jina la Twaha Kiduku lilikuja tu lenyewe kwa sababu mechi yangu ya kwanza nilikuwa nimenyoa Kiduku, sasa wakati wakawa hawajui jina la Twaha wakawa wananiita bondia mwenye Kiduku. “Kiukweli nilikuwa nalichukia sana mwanzoni maana miaka ya nyuma mtu akinyoa Kiduku anaonekana mhuni halafu mimi sina tabia hizo na hata kwenye mechi ya pili sikunyoa Kiduku ila mashabiki wakawa wanashangilia Kiduku…Kiduku.
“Nikaona hili jina limeshakaa na nikawa nikiitwa naitikia hadi nimelizoea na kwa sasa ndiyo limekuwa maarufu zaidi.
Mabondia wengi wamekuwa wakikiri kuwepo kwa mambo ya kishirikina hasa kwa kuwekewa vitu kwenye glavu na wakati mwingine kushindwa kuona, umeshakutana na hali kama hiyo?
“Unajua ninachoamini kila mmoja ana imani yake katika maisha na kama anaimini imani yake inabidi aifuate.
“Ushirikina upo na kwa sisi wenye imani ya kiislam katika hadithi za dini zinasema mtume wetu alirogwa kwa kuhakikisha kuwa uchawi upo lakini Mungu pia ameshusha uchawi, akashusha na kinga ambazo ni dua.
“Sasa kama unaimani ya ushirikina upo basi kinga yake ni kufanya dua na Mungu anavunja kila kitu, watu hawajui tu kwamba Mungu anampenda mja wake pale anapomlilia shida kwa imani yake thabiti hata usiku wa manane.
“Unajua hata katika pambano lililopita na ndugu yangu yaliendekezwa sana mambo hayo kama uliona watu walipanda na mtu mmoja mlemavu akawa anafanya vitu vya ajabu, siyo vizuri ila ni sehemu ya imani yake.
“Kikubwa ni kwamba namshukuru Mungu, kanipandisha na nimefanikiwa kushinda ila mambo mengine naachana nayo nafaya vitu vingine.
Kuna video moja uliposti mtandao ikimuonyesha huyo ambaye unasema alipanda ulingoni kwenye pambano lako dhidi ya Dullah na ukaandika mganga ni Mungu peke yake yeye akitaka liwe lina kuwa. Kwa nini uliamua kuposti ilikuuma?
“Nimeposti hiyo video kwa sababu moja ili mradi watu wamuamini Mungu, Mungu ndiyo kila kitu na ndiyo muweza wa yote.
“Nilikuwa naamka saa nane za usiku naswali, naenda msikitini, nakutana na watu ambao wamejaliwa elimu kubwa ya dini, nikawa nawaomba waniombee dua ya haki na kweli walikuwa wakiniombea.
Niliwahi kupiga stori na bondia mmoja kwamba hataki mapambano na wewe na hata Crown ambayo wewe umeshinda yeye alikuwa akimpelekea mbwa wake baharini kuoga, hii kwako imekaaje?
“Unajua ninachoamini mimi ni nyodo tu, ushaona, kikubwa sitaki kufocus nayo kwa sababu zile clip nimeziona anataka ajibiwe ila mimi naendelea na mazoezi kwa sababu bondia wa kweli unapomtaka lazima akubali mpigane.
“Muwe kama wanaume, mnapigana maisha mengine yanaendelea mbele lakini kila siku inakuwa hivyo maana ugomvi wa wadada na wanaume ni tofauti, wadada mmoja anaweza akamshika mwenzie mara eehee sijui hivi na hivi…dela sijui la kuazima…eeh sijui hivi na hivi.
“Mnajibishana mwisho siku hata kushikana hamshikani ila wanaume mmoja ana-weza akapewa tusi halafu mwingine akamvaa, sasa mambo hayo yakiendelea mimi na huo upande wa pili yatakuwa kama ya wadada…jamani mara hivi mara vile sasa mimi sipo hivyo, siwezi kuongea kama mtoto wa kiume ambayo anaya weza, anajua kazi yake ni ngumi basi mnapigana, mnaendelea.
“Lakini kuwa na magari, magari ndiyo ya kwake kama ana maghorofa ya kwake, watu hatutaki hayo sisi tunachotaka watu waone show hivyo tu, watu wanachotaka kuona ni ladha.
Ukikutana naye pambano utakuwa tayari kupigana?
“Nitakuwa tayari kupigana kwa sababu watu wanataka kuona ladha na siyo mambo mengine, naomba tuongee mambo mengine hiyo mada tuachane nayo.
Una bifu lolote na yeye?
Usikose katika muendelezo wa simulizi ya Twaha Kiduku katika gazeti la Championi Jumatano atakaposimulia namna alivyonusurika kulishwa nyama ya nguruwe kwa sababu ya kiingereza.
IBRAHIM MUSSA, Dar es Salaam