Ufafanuzi wa Somo Jipya Liliongezeka Darasa la 7





KATIBU Mtendaji wa Baraza la Mitihani la Taifa (NECTA), Dkt. Charles Msonde, amesema kuwa idadi ya masomo katika mtihani wa Darasa la Saba mwaka huu imeongezeka kutoka masomo matano hadi sita, somo lililoongezeka linaitwa Uraia na Maadili.

 

Akizungumza John Nchimbi, ambaye ni Afisa Habari wa Baraza hilo kuhusu ufafanuzi wa somo hilo jipya amesema kwamba, somo la Uraia na Maadili si somo geni bali Darasa la Saba wanaoanza mitihani hapo kesho Septemba 8, 2021, waliwahi kuufanya mtihani wa somo hilo wakiwa Darasa la Nne.

 

Aidha, akifafanua zaidi amesema somo hilo ni sehemu ya utekelezaji wa Mtaala Mpya wa masomo uliotolewa na Taasisi ya Elimu nchini ambao uzinduzi wake ulifanyika mnamo mwaka 2014 na utekelezaji wake umeanza kwa Darasa la 7 wanaomaliza masomo yao mwaka huu wa 2021.

 

Katika mitihani hiyo inayoanza kesho kwa nchi nzima na kumalizika kesho kutwa, jumla ya wanafunzi 1,132,143 wa Darasa la Saba watafanya mitihani yao, ambapo kati ya hao wavulana ni 547,502 sawa na asilimia 48.36 na wasichana ni 584,641 sawa na asilimia 51.64

Post a Comment

0 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.

Top Post Ad

Below Post Ad