Taliban Wametangaza Serikali Mpya ya Mpito Nchini Afghanistan





Taliban wametangaza serikali mpya ya mpito nchini Afghanistan, itakayoongozwa na mmoja wa waanzilishi wa kundi hilo, mwanamgambo aliyekuwa akisakwa na FBI kama Waziri wa Mambo ya ndani.
Serikali itaongozwa na Mullah Mohammad Hassan Akhund, huku mwanzilishi mwenza Mullah Abdul Ghani Baradar kama naibu, msemaji wa kundi hilo aliwaambia waandishi wa habari.

''Tunajua watu wa nchi yetu wamekuwa wakisubiri serikali mpya, ''msemaji Zabihullah Mujahid aliongeza.

Taliban ilidhibiti sehemu kubwa ya nchi hiyo zaidi ya wiki tatu zilizopita.

Tangazo la baraza la mawaziri ni hatua muhimu katika kuundwa kwa serikali ya Taliban.

Uteuzi mwingine ni pamoja na Mullah Yaqoob kama kaimu waziri wa ulinzi, na Mullah Abdul Salam Hanafi kama naibu wa pili.

Sarajuddin Haqqani, kaimu waziri mpya wa mambo ya ndani, ndiye mkuu wa kundi la wapiganaji linalojulikana kama Mtandao wa Haqqani.

Tags

Post a Comment

0 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.

Top Post Ad

Below Post Ad