Umoja wa Afrika Umelaani Mapinduzi Nchini Guinea na kulitaka jeshi Kumuachilia Rais Alpha Conde


Umoja wa Afrika umelaani mapinduzi nchini Guinea na kulitaka jeshi kumuachilia Rais Alpha Conde mara moja katika taarifa Rais wa AU, Felix Tshisekedi na Rais wa tume ya AU Moussa Faki wameitisha mkutano wa dharura wa taasisi za umoja huo kuhusu usalama na amani ili kutathmini hali nchini Guinea na kuchukua hatua zifaazo



Hapo jana katibu mkuu wa Umoja wa Mataifa, Antonio Gutteres ametuma ujumbe kupitia mtandao wa twitter akijibu kinachotokea Guinea. Amesema kwamba anafuatilia hali hiyo kwa karibu.

Aliongeza kuwa alilaani kuchukuliwa kwa Serikali kwa nguvu ya bunduki na akataka kuachiliwa mara moja kwa Rais Alpha Conde.

Post a Comment

0 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.

Top Post Ad

Below Post Ad